Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutumie siku ya leo kurejelea ahadi ya kulinda dunia: Ban

Tutumie siku ya leo kurejelea ahadi ya kulinda dunia: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wa siku ya kimataifa ya kuilinda sayari dunia hii leo na kusema kuwa siku hii ni fursa ya watu wote kurejelea wajibu wa pamoja wa kuishi bila kuharibu mazingira wakati huu ambapo sayari hii inakabiliwa na vitisho mbali mbali. Amevitaja vitisho hivyo kuwa ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, matumizi ya rasilimali yasiyo endelevu na matatizo yanayosababishwa na binadamu. Bwana Ban amesema kwa kutishia uwepo wa sayari ya dunia, ni dhahiri binadamu anahatarisha makazi pekee ya mwanadamu na hatma ya uwepo wake, hivyo basi kila mkazi atumie siku ya leo kurejelea ahadi ya kuheshimu sayari ya dunia