Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la misitu latamatika kwa hatua madhubuti:UM

Kongamano la misitu latamatika kwa hatua madhubuti:UM

Kongamano la misitu la Umoja wa mAtaifa limekamilisha kikao chake cha kumi mjini Istanbul Uturuki mapema JUmamosi ya leo kwa kuafikiana hatua kadhaa za kuimarisha udhibiti endelevu wa misitu na kuamua kufikiria hatua ya kuanzisha mfuko maalumu wa hiyari wa kimataifa ili kusaidia kutekeleza muafaka huo.

Kongamanohiloambalo limekutana kwa mara ya kwanza nje ya makao makuu ya Umoja wa MataifaNew Yorklimepitisha maazimio mawili wakati likifunga kikao chake cha wiki mbili.

Moja ya maazimio hayo ni kuhusu misitu na maendeleo ya uchumi ambayo ilikuwa kauli mbiu ya kongamano na pili ni kuhusu ufadhili wa masuala ya misitu.

Kwa kutambua umuhimu wa misitu kwa uhai na maisha nchi wanachama 197 wametoa wito kwa serikali kuchukua hatua mbalimbali ili kuimarisha udhibiti endelevu wa misitu , kuanzia ukusanyaji wa takwimun  hadi kushughulikia sababu za ukataji miti na uharibifu wa misitu.

Pia wakibaini kuwa hakuna suluhisho moja tu la kufikia mahitaji yote ya ufadhili wa misitu kongamano limekubaliana kwamba lazima kuwe na vyanzo vingi vya fedha za ufadhili kuanzia ngazi za kitaifa na kimataifa, sekta za umma na binafsi, na ikiwepo kufikiria kuwa na mfuko wa kimataifa wa hiyari.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kongamanohilokutoka Umoja wa mataifa Jan McAlpine hivi sasa inaeleweka bayana zaidi ya wakati miwngine wowote kuwa misitu ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na maendeleo endelevu.

Zaidi ya theluthi moja ya dunia ukubwa wa dunia na watu bilioni 1.6 duniani wanategemea misitu kwa uhai na maisha yao, huku zaidi ya watu bilioni 3 wanategemea misitu kwa ajili ya kuni za kupikia na kwa kujihifdhi na baridi.

Kongamano hilo limehudhuriwa na watu zaidi ya 50 wakiwemo mawaziri wakuu, makamu wa rais na mawaziri wa misitu na mazingira na maafisa wengine wa ngazi za juu wa serikali.