Wanawake DRC waandamana kupinga kikosi cha waasi

19 Aprili 2013

Wiki hii nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo DRC Kumeshuhudiwa maandamano ya wanawake wakipaza sauti zao kwa jumuiya ya kimataifa hususani ni Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR juu ya hofu ya kufuatia uwepo wa kikosi cha waasi wa ukombozi Rwanda FDRL nchini mwao.

Akina mama hao wanaharakati walikusanyika  eneo la Goma , mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya    Kidemokrasia ya Kongo, wakiwa wamebebea mabango yenye ujumbe wa kupinga uhalifu uliofanywa na kikundi hicho katika majimbo mawili ya Kivu. Ugana na Joseph Msami anayeangazia kilio cha wanawake hawa katika nchi yenye vita kwa miongo kadhaa