Sasa naifahamu fika Syria, mpango wao ndio utakaokwamua nchi yao: Brahimi

19 Aprili 2013

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu katika mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi amesema sasa anaifahamu fika nchi hiyo na kwamba suluhu ya mzozo wa Syria itokane na mpango wa wananchi wenyewe na siyo mpango wake yeye.  Brahimi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjiniNew York, baada ya kupatia baraza la usalama muhtasari wa hali ilivyo nchiniSyriaambapo amesema hali ni mbaya na amerejelea wito aliotoa mwishoni mwa mwezi Januari kuwa barazahilolitie shime suluhu ya mgogoro wa Syria.  Amesema baada ya kubaini kuwa mpango wa suluhu unapaswa kutokana na Wasyria wenyewe, alikuwa na mazungumzo na pande zote zinazopingana nchiniSyria, na amefanya mashauriano na wajumbe wa baraza la usalama hususan Urusi na Marekani.

 (Sauti ya Brahimi)

 “Na wasyria, sikufika popote, Na baraza la Usalama, warusi na wamerekani tulipata maendeleo kidogo lakini bado. Nina furaha kwamba Urusi na Marekani wanazungumza pamoja na pia nina furaha kutokana na majadiliano ya leo, baraza la usalama limetambua kuwa hili ni mgogoro mkubwa kabisa na iwapo wanaamini kuwa wana wajibu wa kusimamia amani na usalama, basi hawana budi kutumia fursa hii na kushughulikia suala hilo kwa umakini zaidi tofauti na walivyofanya hadi sasa.”

 Waandishi wa habari wakataka kusikia kauli yake juu ya uvumi kuwa anajiuzulu na hata wengine kudiriki kudai ya kuwa amebakiza miezi mitatu tu …….

 (Sauti ya Brahimi)

 

“Sijajiuzulu…Kila siku naamka na kufikiria kujiuzulu. Lakini sijafanya hivyo hadi sasa, siku moja nitajiuzulu na bila shaka mtafahamu.”