Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la misitu lafikia ukingoni huko Istanbul

Kongamano la misitu lafikia ukingoni huko Istanbul

Mazungumzo juu ya matokeo ya kongamano kuhusu misitu yanaendelea mjiniIstanbul huku vikao vikitarajiwa kuendelea baadaye leo.Mkurugenzi wa kongamano la misitu la Umoja wa Mataifa Jan McAlpine amewaambia waandishi wa habari kuwa kongamano hili limeweka msingi mpya katika usimamizi wa misitu.

Anasema kuwa usimamizi mwema wa misitu unamaanisha usimamizi wa misitu na miti nje ya misitu ili vyote vichangie kwa maisha ya watu na kwenye uchumi wa jamii na kwa nchi na kutatua masuala mengine ya mazingira yaliyo muhimu.

Bi McAlpine anasema kuwa nchi 197 zilizowakilishwa zinafanya kazi na nyingi zimekuwa kwenye majadiliano  kuhusu maamuzi yaliyofanywa.

Misitu inachukua theluthi moja ya dunia. Zaidi ya watu bilioni 1.6 kote dunia huwa wanategemea misitu kwa maishayao.