Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la jinsia ni muhimu katika kuelewa ustawi wa miji:UNHABITAT

Suala la jinsia ni muhimu katika kuelewa ustawi wa miji:UNHABITAT

Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT linasema miji bora , inayojumuisha wote na yenye ustawi inapaswa kutambua mchango wa kila raia, yaani wanaume, wanawake na vijana.

Hii ni muhimu wakati huu dunia ikikabiliwa na athari za mdororo wa kiuchumi na matatizo ya kifedha ambayo yamesababisha madhara mengi yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, matatizo ya usalama wa chakula na ukosefu wa ajira miongoni mwa wanawake na vijana.

Ripoti ya UN-HABITAT inawasilisha matokeo ya utafiti dhiti ya jinsi watunga sera, wafanya maamuzi, wanazuoni na wakazi wa mijini wanavyolichukulia suala la jinsia na maendeleo ya miji. Ripoti hii ni mchango wa UN-HABITAT katika kutanabaisha matatizo ya wanawake mijini. Shirika hilo linasema sabu za umuhimu wa kuzingatia masuala ya jinsia katika maendeleo ya miji ni moja siku za usoni wakazi wengi mijini watu wazima kati ya miaka 60 na 80 watakuwa wanawake familia nyingi kuongozwa na wanawake.

Pili wakazi wengi wa mijini wanakabiliwa na hali ambazo zinachangia umasikini, hali ambazo zinahusiana na masuala ya jinsia, mfano maji, malazi, usafiri na chakula.

Tatu Wanawake wanatoa mchango mkubwa na muhimu katika masuala ya uchumi kutokana na kipato cha ajira zao. Nne wanwake wengi hawana haki sawa na wanaume kwa masuala kama fursa za kazi, nyumba, afya, na elimu, umiliki wa mali na uwezo wa kutimiza haki zao za msingi.

UN-HABITAT inasema kushughulikia vikwazo hivyo dhidi ya wanawake kutakuwa na faida kubwa kwa familia, serikali na jamii kwa ujumla.