Mkuu wa UNHCR aonya hali mbaya Syria

18 Aprili 2013

 

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Antonio Guterres, amelitahadharisha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba ikiwa mapigano hayataakomeshwa hima nchini Syria, nusu ya raia wa nchi hiyo yaani nilioni 20, watakuwa katika uhitaji mkubwa wa misaada ya kibindamu kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Akilihutubia baraza hilo kwa njia ya video kutoka mjini Geneva Guterres amesema mathalani katika wiki saba zilizopita raia laki nne wamekimbia Syria jambo linalosababisha wakimbizi wa nchi hiyo kufikia zaidi ya milioni moja na laki tatu na kwamba hali hiyo ikiendelea mwishoni mwa mwaka huu huenda idadi ikafikia milioni tatu na nusu huku pia kukiwa na wakimbizi wengine wa ndani milioni sita na nusu ambao wanaweza kuwa wahitaji.

Ametolea wito jumuiya ya kimataifa kunusuru hali hiyo aliyoiita ya kutisha na kuliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba ipo haja kwa serikali kutafuta mbinu mbadala ili kunusuru uwezo wa jumuiya ya kimataifa unaoonekana kuzidiwa na mwitikio wa kimisaada kwa Syria akitolea mfano wa Jordan na Lebanon ambazo zinahudumia wakimbizi wengi kutoka Syria.

SAUTI (GUTERRES)

"Kwa Lebanon mgogoro wa Syria umekuwa tishio kubwa ,idadi ya watu imeongezeka kwa asilimia kumi kwa kuhesabu wakimbizi waliosajiliwa pekee .Wengi wao wanaishi katika maeneo maskini ya nchi. Lakini kimsingi wakimbizi walikuwa hawatafuti usajili. Wafanyakazi wa uhamiaji wa Syria wanakadiria kwamba robo ya idadi ya watu Lebanon yaweza kuwa ni raia wa Syria."