Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwait yataoa ufadhili kwa mashirika yanayotoa huduma nchini Syria

Kuwait yataoa ufadhili kwa mashirika yanayotoa huduma nchini Syria

Serikali ya Kuwait imetoa dola milioni 275 kwa mashirika tisa ya Umoja wa Mataifa yanayotoa huduma za kibinadamu nchiniSyria.Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limepokea dola milioni 110, Shirika la mpango wa chakula duniani FAO dola milioni 40, la kuhudumia watoto UNICEF dola milioni 53 huku Shirika la afya duniani WHO nalo limepokea dola milioni 35.

Ufadhili huu ni sehemu ya ahadi iliyotolewa na taifa la Kuwait wakati wa mkutano kuhusu huduma za kibinadamu uliofanyika mwezi Januari mwaka huu ambapo ahadi za jumla ya bilioni 1.5 zilitolewa. 

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonya kuwa yatapunguza huduma zake nchini Syria ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni kutoka na kuwepo ukosefu wa fedha. Antonio Guterres ni mkuu wa Shirika la UNHCR.

“Wakati idadi ya waathiriwa ikiongeza, wakati idadi ya wanaohama makwao ikiongezeka, uwezo wetu umekuwa mdogo ikilinganishwa na mahitaji. Jitida ziko mbali na kutimiza mahitaji ya watu wa Syria. Tunataka kuwa wazi  kuwa hakuna suluhu ya kibinadamu kwa tatizo hili. Tunaweza kupunguza taabu za watu lakini hakuna suluhu la kibinadamu kwa tatizo hili. Suluhu ni la kisiasa na ndio sababu tumekuwa tukiwaomba wale  walio na majumu ya kisiasa kupata na kubuni njia zitakazowezesha kupatika kwa suluhu la kisiasa.”

UNHCR inasema kuwa hadi karibu wasyria 7000 wanakimbia nchiyaokila siku. UNHCR inakadiria kuwa raia wa Syra walio kwenye mataifa jirani itafikia watu milioni nne mwaka ujao.