Watoto wengi wanaendelea kuuliwa CAR-UNICEF

18 Aprili 2013

Kumekuwa na ongezeko la vifo vya watoto wanaouwawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ikiwemo wale wanaouwawa wakati wakiwa kwenye maeneo ya kucheza na wengine kanisani.Aidha ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF imesema pia makundi mengine ya watoto wamejeruhiwa kufuatia kuongezeka kwa vitendo vya ghasia na unyanyasaji kwa watoto.

UNICEF imeyataka makundi ya kujeshi kusitisha hujuma hizo ambazo imesema kuwa inaweka katika wakati mgumu maisha ya raia wengi kutokana na mashambulizi yanayowafanya na vitendo vya kuwapiga marafuku wahisani wanaosambaza misaada ya usamaria mwema.

Mwakilishi wa UNICEF nchini humo Souleymane Diabate,amesema kuwa hakuna usalama tena kwa watoto kwani hata yale maeneo waliyokuwa wakitumia kucheza sasa yanavamiwa na kufanya uharibifu.