Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu usajili wa umma na takwimu muhimu waanza mjini Bangkok

Mkutano kuhusu usajili wa umma na takwimu muhimu waanza mjini Bangkok

Mkutano wa siku mbili kuhusu usajili wa watu na takwimu muhimu zinazohitajika kuzingatiwa katika mipango ya maendeleo, umeanza leo mjini Bangkok, Thailand. Joseph Msami ana maelezo zaidi kuhusu mkutano huo

(TAARIFA YA JOSEPH MSAMI)

Mkutano huo wa kimataifa umaeandaliwa na Shirika la Afya Duniani, (WHO) na Mtandao wa Takwimu za Afya (HMN), kwa ushirikiano na Kamati ya Umoja wa na unanuia kujadili jinsi ya kuboresha mifumo ya usajili wa umma na takwimu muhimu katika nchi mbalimbali.

Tayari kumekuwa na mikutano ya kikanda barani Asia, Afrika na Mashariki mwa Mediterenia, na mkutano huu utaangazia ubunifu na jinsi ya kuuweka usajili wa umma kwenye ajenda ya maendeleo kimataifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, ni mtu mmoja tu kati ya wanne ndio wanaoishi katika nchi inayosajili zaidi ya asilimia 90 ya uzazi na vifo. Dr. Marie-Paule Kieny ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi kuhusu mifumo ya Afya na Ubunifu katika WHO.

(SAUTI YA Dr. Marie-Paule Kieny)

"Katika nchi nyingi, daftari za mifumo ya usajili wa umma na takwimu muhimu ndizo duni zaidi. Hii ni hali ya aibu, kwani kwa kutojua ni nani amezaliwa, amezaliwa wapi, au nani kafariki dunia na sababu ya kifo, tunawanyima watu uwepo wao. Huu ni ukiukaji wa haki za binadamu, kwani usipowahesabu watu, basi umuhimu wao haupo. WHO inahusika kwa sababu, ili kupanga utoaji wa huduma za afya kwa wote, unahitaji kuwa na mfumo na takwimu za usajili wa umma zinazoaminika”

Takriban nchi 80 hazina mifumo ya usajili wa umma inayoweka daftari za watoto wanaozaliwa na vifo.