Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yaomba Sudan iwezesha misaada kufikia raia

UNAMID yaomba Sudan iwezesha misaada kufikia raia

Mkuu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika nchini Sudan, UNAMID, Mohammed Ibn Chambas amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya ndani wa Sudan. Ibrahim Hamid mjini Khartoum.Katika mazugumzo hayo ameiomba serikali ya Sudan kusaidia UNAMID na misafara ya magari ya misaada kuwafikia raia waliotafuta hifadhi huko Muhajeria na Labado kutokana na mapigano ya hivi karibuni.Halikadhalika ameiomba serikali hiyo kuhakikisha usalama wa raia na mali zao wakati huu ambapo majeshi yake yanajiimarisha kudhibiti ipasavyo miji hiyo baada ya kuitwaa kutoka kwa vikundi vya wapiganaji.

Hata hivyo ameishukuru serikali ya Sudan kwa ushirikiano unaojidhihirisha kati ya polisi huko Darfur na polisi wa UNAMID.

Takribani raia 18,000 bado wamekusanyika kwenye maeneo ya UNAMID karibu na miji ya Muhajeria and Labado tangu tarehe Sita mwezi huu baada ya mapigano kuibuka kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa Sudan Liberation Movement / Minni Minawi na hadi sasa wanasubiri misaada ya kibinadamu.