Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya usalama yarejea Mogadishu: Mahiga

Hali ya usalama yarejea Mogadishu: Mahiga

Hali ya usalama imeripotiwa kurejea mjiniMogadishu, nchiniSomalia, siku tatu baada ya mashambulizi ya kushtukiza mjini humo yaliyosababisha vifo vya makumi kadhaa ya watu na wengine kujeruhiwa. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga ambaye katika mahojiano maalum na Grece Kaneiya wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa amesema hali ya usalama inaendelea kuimarika na ulinzi utaimarishwa bila kuwanyima wananchi haki yao ya kufuatilia masuala ya haki.