UM walaani kuuawa kwa watoa misaada Syria

17 Aprili 2013

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa misaada ya dharura Valerie Amos ametoa rambi rambi kufuatia mfululizo wa vifo vya wafanyakazi wa mashirika ya misaada nchini Syria ambapo mfanyakazi mwingine wa Chama cha halali nyekundu Uarabuni (SARC) Yousef Lattouf ameuwawa.

Bwana Yousef Lattouf anakuwa mfanyakazi wa kumi na nane kuuawa katika mapigano yanayoenedelea nchini Syria ambapo alikutwa na mauti wakati akilinda ghala la SARC katika eneo la Mashahad baada ya ghala hilo kupigwa na kombora April 14, na mfanyakazi mwingine wa kujitolea kujeruhiwa.

Katika salamu zake za rambirambi Bi Amos ameipa pole familia ya Lattouf, na wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu ambao wamekuwa wakikumbwa na mikasa kama hiyo.

Mkurugenzi wa operesheni wa ofisi ya OCHA John Ging, akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa SARC eneo la Allepo , Hail Assi, walizuru eneo la tukio na kulaani kile alichokiita muendelezo wa mashambulizi ya kikatili yanayoendelea kupoteza maisha ya raia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter