Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia ihakikishe usalama wa watendaji wa mahakama: Mtaalamu huru

Somalia ihakikishe usalama wa watendaji wa mahakama: Mtaalamu huru

Serikali ya Somalia na Jumuiya ya kimataifa zimetakiwa kutokatishwa tamaa na mashambulio ya Jumapili na badala yake ziimarishe usalama kwa watendaji wa mahakama ili haki iweze kutendeka, hilo ni tamko la mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kama anavyoelezea Assumpta Massoi.

(Taarifa Assumpta)

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu nchini Somalia, Shamsul Bari, ameitaka serikali ya nchi hiyo na Jumuiya ya kimataifa zisirudi nyuma bali isonge mbele kuimarisha mfumo wa haki licha ya mashambulio ya Jumapili. 

Katika taarifa yake amesema kila wakati anapotembelea Somalia amekuwa akitiwa moyo na vile ambavyo watendaji wa sekta ya mahakama na watoa msaada wa kisheria wamejitolea kufanya kazi licha ya changamoto za usalama.

Bwana Bari amesema ili kuhakikisha utawala wa kisheria na kufanikisha vita dhidi ya ukwepaji wa sheria, watendaji wa mahakama wanapaswa kulindwa ili waweze kufanya kazi yao ipasavyo kwenye nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.

Jengo la mahakama ya kanda ya Banadir lilikuwa moja ya maeneo yaliyoshambuliwa Jumapili na kusababisha vifo vya makumi kadhaa ya watu wakiwemo mahakimu, wanasheria na watu waliokuwa wakifuatilia kesi mahakamani.

Mwakilishi Mkuu wa Katibu Mkuu nchini Somalia Balozi Augustine Mahaiga amezungumza na radio ya umoja

(SAUTI YA BALOZI MAHIGA)