Ofisi ya haki za binadamu ya UM yalaani mashambulizi nchini Somalia

16 Aprili 2013

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani mashambulizi yaliyofanyika tarehe 14 mwezi huu dhidi ya msafara wa misaada karibu na uwanja wa ndege mjini Mogadishu pamoja na mahakama ya mkoa ya Banadir mjini humo ambapo raia 50 waliuawa  wakiwemo watu 35 waliokuwepo mahakamani. Mawakili watatu wakiwemo watetezi wawili maarufu wa haki za binadamu ni miongoni mwa waliouawa kwenye shambulizi hilo. Mawakili hao ni Mohamed Mohamud Afrah mkuu wa chama cha mawakili nchiniSomaliana mwenzake Abdikarin Hassan Gorod ambao kwa miaka mitano iliyopita wamekuwa wa msaada kwa wasomali wengi. Hivi karibuni walitoa msaada kwa mwandishi wa habari Abdiasis Abdinur Ibrahim aliyekamatwa pamoja na mwanamke aliyeripotiwa kukumbwa na kisa cha ubakaji.