Homa ya ndege yaendelea kusambaa China

16 Aprili 2013

Homa ya ndege aina ya H7N9 inaendelea kusambaa nchiniChina, huku vifo vikiongezeka, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO. (TAARIFA YA KANEIYA)

Idadi ya watu ambao wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa homa ya ndege nchini China inazidi kupanda na hadi sasa imefikia vifo 14 kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.

Nao watu 63 wanaripotiwa kuambukizwa maradhi hayo ambayo pia yanafahamika kama (H7N9). WHO inasema kuwa karibu visa 1000 vya ugonjwa vilivyothibitishwa vinafanyiwa uchunguzi wa karibu.

Chanzo ya ugonjwa huo bado hakijulikani hata wakati ndege kama kuku tayari wamepatikana na virusi hivyo. Kundi la wanasayansi wa kiamataifa wantaarajiwa kuwasili nchini China badaye juma hili kuchunuguza hali hiyo na kutoa ushauri. Glenn Thomas ni msemaji wa WHO.

(SAUTI YA GLENN THOMAS)

“Uchina imewaalika wataalam wa kimataifa ili kufanya utafiti kuhusu hali ya homa ya kirusi ya H7N9 nchini humo. Timu hiyo itatathmini mkurupuko huo na jitihada za kukabiliana ili kuelekeza njia za kuzuia na kukabiliana na homa hiyo, na inajumuisha wataalam wa kichina kuhusu magonjwa, utafiti wa maabara na tiba ya kliniki pia kutakuwa na maafisa kutoka Marekani, Muungano wa Ulaya, Australia na WHO.”

WHO inasema kuwa hadi chanzo cha ugonjwa huo kibainike huenda watu zaidi waakaambukizwa.