Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaanza kuwasaidia waathirika wa mafuriko Msumbiji

IOM yaanza kuwasaidia waathirika wa mafuriko Msumbiji

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM limeanza kuzifanyia ukarabati nyumba zilizoharibiwa na mafuriko yaliyoyakumba maeneo mbalimbali nchini Msumbiji katika kipindi cha mwezi Januari mwaka huu.

Kiasi cha familia 5,000 kilipoteza makazi yao kutokana na mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizojitokeza katika eneo la Kusin mwa bara la Afrika.

Ama watu wengine 150,000 waliathiriwa na mvua hizo ambazo chanzo chake kinatajwa kuwa ni mto Limpopo.

IOM pamoja na kuanzisha mpango wa kujenga makazi mapya kwa waathirika hao pia inasambaza huduma muhimu za makazi ambazo zinasaidia kukabiliana na tisho la usalama.

Huduma hizo ni pamoja na simu, taa na vifaa vingine vya makazi.