WFP, TRC yaongeza usambazaji chakula kwa wasyria walioko Uturuki.

16 Aprili 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP likishirikiana na chama cha mwezi mwekundu cha Uturuki  limeongeza mpango wa usambazaji wa chakula kwa makambi ya wakimbizi nchini humo, kwa kuzifikia kambi nyingine nne ambazo zimefurika wakimbizi waSyriawanaokimbia machafuko nchini mwao.Hatua hiyo sasa inafanya jumla ya watu wanaopata msaada huko wa chakula nchini Uturuki kufikia 80,000. Ikilijibu ombi la serikali iliyoomba watu wote wa Syria walioko nchini Uturuki kupatiwa msaada wa chakula  WFP na TRC yalianzisha mpango wa ugawaji wa kadi za kielektronika kwa mamia ya wakimbizi kuanzia wale walioko kwenye kambi ya Adana hadi zile nyingine ikiwemo  Islahiye, Karkamis na Nizipi. Zaidi ya wasyria 190,000 waliyakimbia machafuko nchini mwao, sasa wanapatiwa hifadhi kwenye makambi ya serikali na idadiyaoinaarifiwa kuongezeka kila siku.