Ban alaani mashambulizi ya bomu Mogadishu

15 Aprili 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amelaani vikali mashambulizi yalotekelezwa mjini Mogadishu mnamo tarehe 14 karibu na jumba la mahakama ya kikanda na jingine karibu na uwanja wa ndege, ambayo yanaripotiwa kuwaua watu.

Bwana Ban ameyataja mashambulizi hayo kama vitendo vya kigaidi dhidi ya serikali, taasisi na watu wa Somalia.

Ametum risala ya rambirambi kwa familia walouawa na kuwatakia walojeruhiwa nafuu haraka. Amevipongeza pia vikosi vya AMISOM na jeshi la Somalia, akisema ujasiri na kujitolea kwao kumesaidia kuifanya hali nchini humo kudhibitiwa tena.

Ameelezea imani yake kwamba vitendo hivyo havitoathiri ari ya watu wa Somalia ya kutafuta amani na usalama nchini mwao.