Tubadili mwelekeo wa kushughulikia migogoro: Rwanda

15 Aprili 2013

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amezungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani baada ya ufunguzi wa mjadala kuhusu uzuiaji wa migogoro barani Afrika na kusema wakati umefika Umoja wa Mataifa ubadili mwelekeo wa kushughulikia masuala hayo.

Bi. Mushikiwabo ambaye nchi yake inashika kiti cha Urais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Aprili, amesema Rwanda inaamini kuwa jitihada zaidi zinapaswa kuelekezwa kwenye kupatia suluhu mizizi ya migogoro.

(SAUTI Louise-1)

Waziri Mushikiwabo akaenda mbali zaidi na kuzungumzia mtazamo wake kuhusu brigedi inayokwenda Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC kwa mujibu wa azimio la baraza la usalama kujibu mashambulizi iwapo waasi watahatarisha usalama wa raia.

(SAUTI Louise-2)