Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni lazima tuboreshe maisha ya watu maskini: UN-Habitat

Ni lazima tuboreshe maisha ya watu maskini: UN-Habitat

Kikao cha 24 cha Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na nyumba na makazi (UN Habitat), kimeanza leo mjini Nairobi, huku viongozi wakitoa wito wa kuboresha maisha ya watu maskini duniani.

Akifungua kikao hicho, rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta, mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa yanatakiwa kutumia fursa ya kikao hicho cha wiki moja kutafakari kuhusu changamoto zinazoyakumba makazi ya mijini na kujadili njia za kukabiliana nazo.

Mkurugenzi Mkuu wa UN-Habitat, Dr Joan Clos, amesema jinsi vijiji na miji itakavyoendelezwa katika wakati mfupi ujao, itachangia kwa kiasi kikubwa viwango vya maisha ya baadaye vya mamilioni ya watu. Amewakumbusha wanaoshiriki mkutano huo kuwa mnamo Aprili 5, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitoa wito kasi iongezwe na serikali, mashirika ya kimataifa na yale ya umma ili kuyafikia malengo ya maendeleo ya milenia ifikapo mwaka 2015.

Mshauri maalum wa Katibu Mkuu kuhusu mipango ya maendeleo baada ya 2015, Bi Amina J Mohammed, amesema kipindi cha siku 1000 kinatoa nafasi ya kuzingatia umuhimu wa kukamilisha kazi ili kutimiza malengo ya maendeleo. Kuhusu viwango vya makazi, amesema bara la Afrika limepiga hatua, ingawa bado kuna kazi nyingi ya kufanya.

(CLIP ya AMINA MOHAMMED)