Biashara ya urembo yamwezesha mkimbizi kujitegemea

15 Aprili 2013

Mwanamke mmoja mkimbizizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambae sasa anaishi Uganda ameweza kutimiza ndoto yake ya kujitegema kupitia biashara ya urembo. Mwanamke huyo Rosetta Wabenga ambae ni mama wa watoto watatu anasema kuwa amepitia mengi lakini sasa kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema amepata mafanikio .

Anasema mara ya mwisho kumuona bwanake ambaye alikuwa ni mwanaharakati ni mwaka 2006 alipochukuliwa na watu waliokuwa na silaha. Wabenga ambaye sasa ana umri wa miaka 17 alikimbia nyumbani na kuingia nchini Uganda na kutafuta msaada kwa shirika la InterAid linalofadhiliwa na UNHCR . Kwa muda wa miaka miwili Wabenga hakukata tamaa hata baada ya kutekwa nyara na kubakwa na watu ambao hadi sasa hawajafikishwa mbele ya sheria mjini Kampala. Lakini mwishowe aliweza kupata mkopo kutoka kwa Shirika la InterAid wa dola 320 na kunzisha dula la uembo wa nywele.