Baraza Kuu lafanya mjadala kuhusu udhibiti wa uchumi wa kimataifa

15 Aprili 2013

Wakati harakati za kubuni vigezo vya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 zikiendelea, mjadala umefanyika leo katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu udhibiti wa uchumi wa kimataifa.Wakati wa mjadala huo, rais wa Baraza Kuu, Vuk Jeremic, amesema kuwa kulingana na makubaliano ya Rio+20, sera zinazotungwa kwa ajili ya kuendeleza ukuaji wa kiuchumi zinatakiwa kujumuishwa katika maendeleo ya kijamii na mazingira, kama sehemu ya maendeleo endelevu.

 Katika hotuba yake, Bwana Jeremic ametoa wito kuwepo ushirikiano ili kutokomeza umaskin

(SAUTI YA VUK JEREMIC)

“Ili tuwe na ajenda ya kina ya baada ya mwaka 2015 katika siku elfu moja zijazo, na ambayo ni ya pamoja na inayojumuisha wote juhudi endelevu zitahitajika ili kuhakikisha kuwa maamuzi ya wahusika muhimu kimataifa yanauiana vyema na yale yanayofanyika katika Umoja wa Mataifa. Tushirikiane kupunguza pengo la kiuchumi kati ya maskini na matajiri, na kutokomeza umaskini katika enzi ya sasa. Haya ndiyo matarajio ya ajenda ya maendeleo baada ya 2015: kuhakikisha hadhi ya kila mtu. Kufikikia lengo hili ni sababu muhimu kwetu kujitahidi kuboresha mfumo wa udhibiti wa uchumi wa kimataifa."