Tanzania yajiandaa kupeleka askari DRC

15 Aprili 2013

Harakati za maandalizi ya brigedi ya kusaidia ulinzi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC zinaendelea ambapo nchi husika zinakamilisha shughuli hiyo miongoni mwao ni Tanzania kama anavyoripoti Assumpta Massoi.(Ripoti yaAssumpta)

Takribani mwezi mmoja baada ya Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuupatia ujumbe wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, uwezo wa kuwa na brigedi ya kujibu mashambulizi iwapo waasi watahatarisha usalama wa raia, Tanzania ambayo ni moja ya nchi itakayopeleka askari imesema inajiandaa kupeleka kikosi chake cha kulinda amani.

Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa wamekubaliana na Umoja huo kwamba hadi kufikia mwezi ujao vikosi hivyo viwe vimekwishawasili DRC.

(SAUTI MANONGI)

Nchi zingine zinazounda brigedi hiyo ya MONUSCO ni Malawi, Kenya na Afrika Kusini.