Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahiga ashtushwa na mashambulizi Mogadishu

Mahiga ashtushwa na mashambulizi Mogadishu

Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dkt. Augustine Mahiga ameelezea kushtushwa kwake na kulaani mashambulizi yaliyofanywa mjini Mogadishu nchini Somalia siku ya Jumapili na kusababisha vifo vya watu Kumi na Tisa huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongeza.

Balozi Mahiga ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa wasomali na jumuiya ya kimataifa wasikatishwe tama na tukio hilo huku akituma rambi rambi kwa wafiwa na kuwatakia uponaji wa haraka waliojeruhiwa.

(SAUTI YA MAHIGA )