Skip to main content

Kumbukumbu ya Hammarskjöld yamulika usalama wa walinda amani

Kumbukumbu ya Hammarskjöld yamulika usalama wa walinda amani

Ni wiki chache tu zimesalia hadi Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa, mnamo Mei 29. Kazi ya kulinda amani ni kazi inayohitaji ujasiri na kujitolea, kwani aghalabu kazi hii hufanyika katika maeneo na mazingira yasiyo salama.

Mnamo siku ya Jumatano wiki hii, Umoja wa Mataifa ulifanya hafla maalumu ya kumkumbuka na kumuenzi Dag Hammarskjöld, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa tokea Aprili 10 1953 hadi Septemba 1961.

Bwana Hammarskjöld alikumbana na mauti yake wakati akiwa kwenye shughuli zinazohusiana na kutafuta amani. Na mapema wiki hii, walinda amani wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini wameuawa katika shambulizi la kuvizia. Ungana na Joshua Mmali katika makala hii inayomulika matukio ya wiki hii na yale ya kihistoria