Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WMO yaondoa jina la Sandy kwenye orodha ya vimbunga

WMO yaondoa jina la Sandy kwenye orodha ya vimbunga

Shirika la hali ya hewa duniani, WMO limeamua kuondoa rasmi jina Sandy katika orodha ya vimbunga vinavyopiga bahari ya Atlantiki.

Uamuzi huo unafuatia kimbunga Sandy kusababisha madhara makubwa huko Jamaica, Cuba, Haiti na baadhi ya maeneo ya kati nchini Marekani, mwezi Oktoba mwaka jana.

Msemaji wa WMO Claire Nullis akizungumza mjini Geneva, Uswisi amesema nafasi ya Sandy itachukuliwa na jina Sara kuanzia mwaka 2018.

Kimbunga Sandy kilisababisha vifo vya watu Milioni 300 na hasara ya kiuchumi ya dola zaidi ya Bilioni 65. WMO imesema kimbunga hicho pamoja na madhara yake kimekuwa fundisho kubwa katika nyanja za utabiri wa hali ya hewa, utoaji wa taarifa za dharura na mawasiliano.