Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatuwezi kuwa na ukuaji unaojali mazingira bila kuhifadhi bahari: FAO

Hatuwezi kuwa na ukuaji unaojali mazingira bila kuhifadhi bahari: FAO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, José Graziano da Silva, amesema leo ya kwamba, juhudi za kutokomeza njaa na kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi katika visiwa vya Pasifiki zitategemea ufanisi wa maendeleo endelevu, pamoja na matumizi yenye busara ya mabahari na uvuvi. George Njogopa ana maelezo zaidi(TAARIFA YA GEORGE)

Mkurugenzi huyo Graziano amesema kuwa dunia haiwezi kuwa na uchumi  wa kijani yaani unaojali mazingirakamakutakosekana kile alichokiita uchumi bluu ambao ndiyo inasababisha kuwepo kwa maendeleo endelevu ikiwemo kwenye maeneo ya baharini kunakopatikana rasilimali za uvuvi.

Alisema kuwepo kwa usimamizi kwenye maeneo ya uvuvi, hakuwezi kupuuzwa kwani hutegemewa na zaidi ya watu billion 3, ambao kimsingi huchukua asilimia 15 ya ulaji wa protein.

Lakini pia alieleza namna hali hiyo inavyofadisha watu kwa kuanzisha ajira ambayo kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa kiasi cha ajira milioni 200 hutengenezwa duniani kote.

Akizungumza kwenye mkutano wa Mawaziri wa kilimo, Mkurugenzi huyo alisema kuwa suala la kukabiiana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi ni suala linalojali zaidi maisha ya binadamu kama ilivyo kwa kukabiliana na janga la njaa.