Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Anga za juu ni pahala pa wote; wasichana wajifunze hesabu na Sayansi: Anousheh

Anga za juu ni pahala pa wote; wasichana wajifunze hesabu na Sayansi: Anousheh

Wakati leo ni siku ya kimataifa ya kuadhimisha siku ambayo chombo cha kwanza kikiwa na binadamu kilienda anga za juu, mmoja wa wahandisi wanawake nchini Iran ambaye amewahi kwenda anga za juu kutembea na kujifunza Bi. Anousheh Ansari amesema watoto wa kike wajifunze hesabu na sayansi zaidi ili waweze kufuata nyayo za mwanamke wa kwanza kwenda anga za juu Valentina Tereshkova.

Bi. Ansari amesema hayo katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA Bi. ANSARI)

Chombo cha kwanza angaza juu kilirushwa na Yuri Gagarin wa Urusi tarehe 12 Aprili mwaka 1961.