Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

G-8 yaunga mkono jitihada za UM dhidi ya ukatili wa kingono

G-8 yaunga mkono jitihada za UM dhidi ya ukatili wa kingono

Unaweza kuelezea vipi mantiki ya kunajisiwa watoto wenye umri wa kati ya miezi Sita hadi mwaka mmoja? Hiyo ni hoja aliyoitoa Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya ukatili wa kingono kwenye migogoro, Zainab Hawa Bangura alipohutubia mawaziri kutoka kundi la G8, huko London, Uingereza walipokutana kupitisha azimio la kuzuia ukatili wa kingono kwenye mizozo.

Bangura amesifu hatua ya nchi hizo na kusema sasa mbio za watuhumiwa wa vitendo hivyo zinafikia ukingoni kwani azimio hilo limedhihirisha kuwa ukatili wa kingono ni tishio kwa amani na usalama duniani.

Kupitia azimio hilo, nchi hizo ambazo ni Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Urusi, Uingereza na Marekani zimeahidi kuchukua hatua madhubuti kusaidia wahanga wa ukatili wa kingoni vitani, kuzuia vitendo hivyo kutokea na kuhakikisha watuhumiwa wanawajibishwa.

Kutekeleza ahadi yao kundi hilo la nchi tajiri duniani limeahidi dola Milioni 36 ambapo Bi. Bangura ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka.

(SAUTI BANGURA)

Mwakilishi huyo maalum wa Katibu Mkuu akaenda mbali zaidi na kueleza hisia zake kwa nchi kuchukau hatua dhidi ya ukatili wa kingono.