Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban afanya mkutano na rais wa Serbia Tomislav Nikolić

Ban afanya mkutano na rais wa Serbia Tomislav Nikolić

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na rais wa Jamhuri ya Serbia Tomislav Nikolić ambapo walizungumzia mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu wajibu wa mahakama ya kimataifa ya uahlifu wa kivita kenye mapatano.Katika mazungumzo hayo Bwana Ban alirejelea kauli alioitoa kwenye mkutano huo ya kwamba Umoja wa Mataifa umejizatiti kuendelea kuunga mkono kazi za mahakama za kitaifa na zile za kimataifakamavyombo muhimu vya kuepusha wakosaji kukweka mkono wa sheria.

Ban pia alitumia fursa hiyo kuelezea matumaini kuwa mataifa ya Serbia na Kosovo yatataendelea na mazungumzo chini ya Jumjuiya ya ulaya ili kupata matokeo yaliyo mazuri.