Kirusi aina ya A(H7N9) cha watia kiwewe wataalamu wa afya

11 Aprili 2013

Shirika la kimataifa linalohusika na afya ya wanyama, OIE limekumbwa na sintofahamu juu ya ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege ya kirusi aina ya A(H7N9) ambacho hadi sasa kimesababisha vifo vya watu Kumi nchini China.

Sintofahamu hiyo inatokana na taarifa ya kwamba kuku waliothibitika na kirusi hicho na pia kushukiwa kuwa chanzo cha maambukizi kwa binadamu hawana dalili dhahiri za ugonjwa huo.

Mkurugenzi Mkuu wa OIE Dkt. Bernad Vallat amesema kwa kuzingatia taarifa hizo kwa sasa wanakabiliwa na mazingira ya kipekee kwani wanashughulikia kirusi cha homa ya mafua chenye uwezo mdogo wa kusababisha ugonjwa kwa kuku lakini kina uwezo wa kusababisha ugonjwa hatari kwa binadamu.

Hata hivyo amesema shirika lake linashiriki vilivyo katika jitihada za kimataifa za kudhibiti hatari mpya zitokanazona kirusi hicho.