Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misitu na sekta ya misitu vyachangia uchumi unaojali mazingira

Misitu na sekta ya misitu vyachangia uchumi unaojali mazingira

Kuna haja ya kuweka vyema kumbukumbu za mchango wa kijamii na kiuchumi utokanao na misitu kwa maendeleo ya binadamu .

Hayo yameelezwa leo katika kongamano la Umoja wa Mataifa la mistu linaolendelea huko Istanbul Uturuki.

Kongamanohilolinafanyika katika wakati muafaka hasa ukizingatia matokeo ya mkutano wa Rio+20 na mapendekezo ya kongamano hilo kuhusu ufadhili na maendeleo ya kiuchumi yatokanayo na misitu.

Akizungumza katika kongamanohilomkurugenzi mkuu msaidizi wa idara ya misitu kwenye shirika la FAO Edouardo Rojas-Briales amesema kongamanohilolitaweka muongozo wa kupitia mipango ya kimataifa kuhusu misitu.

(SAUTI EDUOUARDO ROJAS-BRIALES)

“Amesema utafiti unaonyesha kwamba mchango wa misitu na sekta ya misitu katika uchumi unaojali mazingira , kupunguza umasikini na maendeleo endelevu unatambulika zaidi kuliko awali. Tunahitaji hatahivyo kuweka kumbukumbu vizuri na ketanabaisha vilivyo mchango wa kijamii na kiuchumi unaofanywa na misitu kwa maendeleo ya binadamu”

Bwana Rojas-Briales amesema ajenda ya kongamano la Umoja wa Mataifa la Mmisitu limeandaliwa ili kushughulikia masuala mbalimbali ya misitu, matumizi yake na mchango wake muhimu kwa uchumi.