Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umetoa wito kuongeza vikosi vya usalama, Somalia

UM umetoa wito kuongeza vikosi vya usalama, Somalia

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuongezwa vikosi vya usalama nchini Somalia kwa ajili ya kukabiliana na masuala na wanamgambo wa kundi la alshaabab ambao hivi karibuni walisambaratishwa katika ngome zao.Wito huo umetolewa na Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga wakati alipokutana na waandishi wa habari jijiniDar es salaam kuelezea hali ya usalama ya nchi hiyo.

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Kwa kiwango kikubwa nguvu za kundi la alashaabab zimesambaratishwa kufutia operesheni iliyoendeshwa na vikosi vyaUgandanaBurundiambavyo viliitika mwito wa Umoja w Mataifa na Umoja wa Afrika iliyotaka msaada wa kujeshi kukabiliana na uasi uliokuwa ukiendeshwa na kundihilo.

Hata hivyo Balozi Mahiga anaona kuwa bado eneo hilo linakabiliwa na kitisho cha kuzuka mashambulizi ya kufizia kutoka kwa masalia ya askari wa kundi hilo,na hivyo amehimiza haja ya kuongezw askari wa kuimarisha hali ya usalama pamoja na kusaka silaha zilizotelekezwa  na wanamgambo hao.

Mzozo wa usalama nchini Somalia ulizuka tangu mwaka 1991 wakati uliopoangushwa utawala wa kijeshi wa Siad Barre na baadaye mzozo huo kusambaa nchi nzima.

Kukosekana na serikali thabiti pamoja na kuchelewa kuingia kwa Jumuiya ya Kimataifa nchini humo, kulitoa nguvu kwa makundi ya wanamgambo kujiimarisha na kufaulu kudhibiti maeneo yote muhimu.

Katika jitihada za kuleta utengamano zaidi, mapema mwezi ujao kunatazamiwa kufanyika mkutano maalumu ambao pamoja na mambo mengine unatazamia kujadiia agenda ya usalama.

Mkutano huo uliotishwa na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroun ambao utafanyika London unatazamia kuwaleta pamoja wahisani pamoja na Umoja wa Mataifa wenyewe.

(SAUTI MAHIGA)

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa, Somalia inaanza kurejea katika hali ya utulivu na amani baada ya kuwepo kwa serikali mpya  ambayo imepewa majukumu ya kuandaa mazingira kwa ajili ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwaka