Ban kuwa na mazungumzo na Obama hii leo

11 Aprili 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon baadaye hii leo atakuwa na mazungumzo na Rais Barack Obama hukoWashingtonDC.

Miongoni mwa ajenda za mazungumzoyaoni hali ya sintofahamu huko rasi yaKoreawakati huu ambapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu waKoreainaendeleza vitisho vya kutaka kufanya jaribio la silaha za nyuklia kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama.

Masuala mengine yanayotarajiwa kujadiliwa ni ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Marekani.

Mapema jana Bwana Ban alikuwa na mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Serbia Tomislav Nikolić, ambapo amemsisitizia kuwa Umoja wa Mataifa umejizatiti kuendelea kuunga mkono kazi za mahakama za kimataifa na zile za kimataifakamavyombo muhimu vya kuepusha wakosaji kukweka mkono wa sheria.