Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahuzunishwa na tetemeko la ardhi huko Iran

Ban ahuzunishwa na tetemeko la ardhi huko Iran

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehuzunishwa na maafa na uharibifu wa mali uliosababishwa na tetemeko la ardhi la ukubwa wa Sita nukta Tatu katika kipimo cha richa hukoIran.Ban ametuma rambi rambi zake  kwa serikali ya  Iran na kwa watu waIranna familia zilizopoteza jamaa.

Bwana Ban amesema Umoja wa mataifa uko tayari kuandaa msaada wowote wa kimataifa unaohitajika kufuatia tetemekohilo.