Malawi kupunguza uzalishaji wa gesi chafu itokanayo na ukataji miti

10 Aprili 2013

Malawi ni moja ya nchi nne za Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC kuwa na mpango maalumu wa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu itokanayo na ukataji mitina uharibifu wa misitu, yaani REDD, pia ufuatiliaji, utoaji taarifa na uthibitishaji wa suala hilo.

Hayo yamesemwa na waziri wa mazingira na udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa wa nchi hiyo Jenifer Chilunga kwenye kongamano la Umoja wa Mataifa la misitu linaloendelea Istanbul Uturuki.

(SAUTI YA JENIFER CHILUNGA)

Wakati huo huo kongamano hilo la mistu limetoa tuzo za 2012/2013 za Umoja wa Mataifa za misitu kwa watu.

Washindi wa tuzo hizo zilizoanza mwaka 2011 ni  Rose Mukankomeje kutoka Rwanda; Preecha Siri kutoka  Thailand; Almir Narayamoga Surui wa  Brazil; Hayrettin Karaca wa Uturuki na Ariel Lugo wa Marekani