Mkutano ni hatua ya kwanza ya kuhakikisha kuwa sauti za wanawake kutoka eneo la Sahel zinasikika na kuwa maoni yao yanatiliwa maanani. Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Sahel Romano Prodi anasema kuwa wanawake katika eneo la Sahel watakuwa kiungo muhimu katika utulivu wa eneohilo. Mjumbe kutoka kwa Jumuiya ya Ulaya Catherine Ashton anasema kuwa wakati mwanamke anapopiga hatua jamii nazo hupiga hatua , penye wanawake huteseka jamii huteseka pia. Mapendekezo ya mkutano huo yatawasilishwa kwemye mkutano wa wafadhili utakaondaliwa mjiniBrussels. Kati ya mapendekezo yaliyowekwa kuhakikisha kuwepo amani , usalama na maendelo eneo laSahelwashiriki walisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa asilimia 30 ya washiriki wa kutoa maamuzi ni wanawake.