Kudorora kwa kiwango cha ukuaji biashara kutaendelea kushuhudiwa 2013:WTO

10 Aprili 2013

Kiwango cha ukuaji wa biashara katika mwaka 2012 kinaripotiwa kufikia asilimia 2.0 ikiwa ni chini dhidi ya kile kilochoshuhudiwa mwaka mmoja nyuma yaani 2011 ambacho kilikuwa kwa asilimia 5.2.

Hali hiyo ya kusua sua kwa kukua kwa biashara duniani inatazamiwa pia kushuhudiwa mwaka huu 2013,ambako kiwango chake kinatazamia kufikia asilimia  .3 3 huku bara la Ulaya likiendelea kurejesha nyuma kiwango cha uingizaji bidhaaa.

Kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na shirika biashara duninia WTO imesema kuwa kiasi kidogo cha ukuaji wa biashara katika mwaka 2012, ni matokeo ya msuko suko wa uchumi ulioikumba dunia katika miaka ya hivi karibuni. Ripoti hiyo imesema kuwa bado hakukuchukuliwa jitihada za kutosha kukabiliana na matokeo ya mwamo wa uchumi wa dunia.

George Njogopa na taarifa kamili

Kushuka kwa kiwango cha ufanyaji biashara katika kipindi cha mwaka 2012, kumefungamanishwa pia na hali ya kudorora kwa uchumi katika mataifa yaliyopiga hatua kimaendeleo hasa barani Ulaya.

 Baadhi ya mambo yaliyotajwa na ripoti hiyo ni pamoja kuongezeka tatizo la ajira katika nchi zilizoendelea jambo ambalo lilisababisha kushuka kwa kiwango cha uingizaji wa bidhaa.

Hali hii ilisababisha kushuka kwa kasi maingiliano ya kibiashara baina ya mataifa yaliyoendelea nay ale yanayoinukia kiuchumi, kwani pande zote hazikusafirish nje bidhaa za kutosha.

Ripoti hiyo imeangazia hali ya uchumi kwa Marekani ikisema kuwa uchumi wake unatazamia kufanya vyema katika kipindi cha mwaka 2013 na hii itachangia na kusua sua kwa uchumi wa bara la Ulaya.