Je Maendeleo ya hali ya mtoto katika nchi tajiri yako hatarini? UNICEF

10 Aprili 2013

Utafiti uliozinduliwa leo na ofisi ya utafiti ya shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuhusu maendeleo ya hali ya mtoto katika mataifa tajiri , umebaini kwamba Uholanzi na nchi zingine nne za zikiwemo za Scandnavia za Finland, Iceland, Norway na Sweden kwa mara nyingine zinashika nafasi ya juu katika orodha huku nnchi nne za Ulaya Kusini ikiwemo Ugiriki, Italia , Ureno na Hispania ziko katika nafasi za chini za orodha hiyo. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Utafiti huo ulioitwa ripoti card 11 kutoka UNICEF umeangalia kwa kina hali ya watoto katika mataifa yote yaliyoendelea kiviwanda .

Wakati mjadala ukiendelea kutoa maoni tofauti ya athari na faida za hatua kali zinazochukuliwa kukabiliana na mdororo wa uchumi na kupunguza matumizi utafiti huo umeelezea mafanikio ya mataifa 29 yaliyoendelea katika kuhakikisha hali bora ya maisha ya watoto katika muongo wa kwanza wa karne hii.

Ulinganishaji wa kimataifa wa hali ya watoto kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kudhihirisha kwamba umasikini wa watoto unaweza kuepukika lakini sera bora hazijatumika katika nchi zote, na kwamba baadhi ya nchi zinajitahidi zaidi ya zingine katika kuwalinda watoto wao. Chris de Neubourg ni mkuu wa sera za kijamii na kiuchumi wa ofisi ya utafiti ya UNICEF

(SAUTI YA CHRIS DE NEUBOURG)

Naye mkurugenzi mkuu wa ofisi hiyo ya utafiti ya UNICEF Gordon Alexander amesema iwe ni wakati wa mdororo wa uchumi au wa ki[pindi kizuri ya kifedha UNICEF inazitaka serikali zote na washirika wa masuala ya kijamii kuzingatia maslahi ya watoto na vijana wakati wafanya maamuzi.