Taa za kutumia nishati ya jua kukabiliana na ubakaji Somalia
Katika kupambana na ukatili wa kijinsia nchini Somalia, Shirika la kimataifa la masuala ya umeme la nchini Japan, Panasonic, kwa kushirikiana na shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM, limeanzisha utafiti wa namna taa za kutumia nishati ya miale ya jua zinavyoweza kupunguza ukatili huo katika kambi za wakimbizi na wahamiaji . Mchango huo wa kiasi cha dola za Marekani elfu 31 unafuatia uchunguzi usio rasmi wa IOM wa mwaka 2012 ulioonyesha kuwa asilimia kubwa ya vitendo vya ukatili ikiwamo ubakaji hufanyika usiku katika makambi wakati kukiwa na giza . Joseph Msami amefanya mahojiano na msemaji wa shirikia la kimataifa la uhamiaji IOM Jumbe Omari Jumbe ambaye anaanza kwa kueleza nini hasa shirika hilo litafanya katika utafiti huo wa kisayansi unaolenga kupambana na ukatili wa kijinsia katika nchi ambayo kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji, ubakaji unaripotiwa kwa kiwango cha juu kuliko nchi nyingine duniani. (MAHOJIANO)