Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaendelea kuubeba mzigo wa wakimbizi wa DRC Uganda

UNHCR yaendelea kuubeba mzigo wa wakimbizi wa DRC Uganda

Umoja wa Mataifa unaendelea na juhudi za kuwasaidia wakimbizi wanaosababishwa na mapigano katika nchi mbalimbali, kama vile nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo hali inaripotiwa kuendelea kuwa tete na kusababisha maelfu ya raia kukimbilia nchi jirani kutafuta hifadhi.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi hadi sasa takribani raia milioni 2 na laki mbili wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni wakimbizi. UNHCR inasema raia laki nne wa DRC  wamevuka mpaka kutafuta hifadhi huku nchini Uganda takwimu zikionyesha idadi ya wakimbizi elfu sabibni katika nchi hiyo iliyoko Mashariki mwa Afrika.

Ungana na Joseph Msami anayeangazia namna UNHCR na washirika wanavyiosaidia kuhudumia maelfu ya wakimbizi nchini Uganda.