Mwandishi wa UNMISS amuua mkewe na kujiua

9 Aprili 2013

Mwandishi wa habari aliyekuwa akifanya kazi katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili yaSudanKusin UNMISS amejiua baada ya kutuhumiwa kuwa alimuua mkewe. Mke wa mwandishi huyo wa habari wa redio naye pia alikuwa ameajiriwa katika kituo alichokuwa akifanyia kazi mumewe. Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja chanzo cha matukio hayo na maafisa wa polisi walikuwa bado wakichunguza sababu ya kutokeza kwa hali hiyo. Mmoja ya mtu wa karibu wa waandishi hao ambaye anafanya kazi na kituo cha redio cha Miraya alielezea kusikitishwa juu ya matukio hayo lakini hakueleza zaidi.