Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU  yazindua shindano kwa wabunifu vijana

ITU  yazindua shindano kwa wabunifu vijana

Shirika la kimataifa la mawasilino ITU limezindua shindano lake ambalo hufanyika kila mwaka kwa shabaha ya kuchochea ubunifu kwenye sekta ya habari, mawasiliano na teknolojia. Washiriki wa shindano halo wanatakiwa kubuni miradi ya ujasilia malikupitia teknolojia ya mawasiliano na kisha kiwakilisha kwa jopo la wataalamu wa ITU wataokutana Novemba mwaka huu huko Bangkok. Shindano hilo ni la wazi kwa washiriki wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 26 linatoa fursa za ajira na wakati huo huo kuwasukuma washiriki kuwa wabunifu kwa kuangazia changamoto zinazoikabili dunia kwa sasa.