Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa madawa wawasili kwenye Jamhuri ya Afrika kati

Msaada wa madawa wawasili kwenye Jamhuri ya Afrika kati

Ndege maalum ya shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ikiwa imesheheni  tani 23 za madawa na matenki ya maji imewasili jana kwenye taifa linalokumbwa na mzozo la Jamhuri ya Afrika ya kati, majuma mawili baada ya waasi kuchukua uongozi wa taifahilo. Msaada huo unaojumuisha bidhaa muhimu  kwenda Jamhuri ya Afrika ya kati unafuatia majuma kadha ya hali mbaya ya usalama na uporaji wamaliambapo mahospitali na vituo vya afya vilishuhudia hasara kubwa ya madawa na bidhaa zingine. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO