Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 85 wameuawa huko Jongley, Sudan Kusini

Zaidi ya watu 85 wameuawa huko Jongley, Sudan Kusini

Ripoti ya Umoja wa Maataifa iliyochapishwa Ijumaa iliyopita inaonyesha kuwa karibu watu 85 waliuawa wakati wa uvamizi dhidi ya kundi moja la wafugaji karibu na eneo la Walgak kwenye jimbo la Jonglei tarehe 8 mwezi Februari mwaka huu wengi wakiwa ni wanawake na watoto. Assumpta Massoi anaripoti.

(PKG YA ASSUMPTA)

Kulingana na uchunguzi uliongoza na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchiniSudanKusini UNMISS kati ya tarehe 11 mwezi Februari na machi mosi ulibaini kuwa watu 85 waliuawa ambapo 69  katiyaowalitambuliwa. Watu wengine 37 walijeruhiwa  huku wengine  34 wakiwa hawajulikani waliko wakati wa uvamizi ulio mbaya zaidi kushuhudiwa kwenye jimbo la Jongley tangu mwanzo wa mwaka huu. Kundi la wanaume waliokuwa wamejihami wanaokisiwa kuwa kutoka  kabila la Murle waliwavamia wafugaji kutoka jamii ya Lou Nuer walipokuwa wakielekea malishoni. Kundi la wanajeshi 40 kwa kikosi cha SPLA walitumwa kuwalinda wafugaji hao lakini walizidiwa. Cecile Pouly ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa

(Sauti ya Cecile Pouly)

“Tunatoa wito kwa utawala wa Sudan Kusini kuanzisha uchunguzi mara moja kwenye uvamizi huu na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika ili kumaliza  visa kama hivi pamoja na ukwepaji wa sheria”