Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wakimbizi wa Syria kuzidi kuongezeka: UNHCR

Idadi ya wakimbizi wa Syria kuzidi kuongezeka: UNHCR

Idadi ya raia wa Syria watakaotafuta hifadhi nchi jirani kwa mwaka huu wa 2013 inatarajiwa kuongezeka na kufikia Milioni Nne iwapo mzozo unaoendelea hivi sasa nchini mwao hautapatiwa suluhisho la kisiasa.

Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR limesema kuwa hadi sasa Jordan, Uturuki, Lebanon na Iraq kwa jumla wanahifadhi wakimbizi zaidi ya Milioni Moja nukta Tatu wa Syria na kwamba uhaba wa fedha unakwamisha usaidizi wa kibinadamu kwa raia hao.

UNHCR imesema mashirika ya misaada yameomba dola Bilioni Moja kwa ajili ya operesheni hiyo lakini hadi sasa yamepata dola Milioni 300 pekee.

Panos Moumtzis, afisa kutoka UNHCR amesema ukata unasababisha watoe misaada michache hali inayoweka hatarini maisha ya wanawake na watoto.

(SAUTI YA PANOS)