Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la awali la uchunguzi Syria kuondoka ndani ya saa 24

Kundi la awali la uchunguzi Syria kuondoka ndani ya saa 24

Kikundi tangulizi cha kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchiniSyriakinahitimisha maandalizi yake hukoCyprustayari kuelekea nchini humo ndani ya Saa 24. Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliyoitoa huko The Hague, Uholanzi kando ya mkutano unaojadili mkataba wa kimataifa wa kudhibiti silaha za kemikali. Bwana Ban amesema tayari jopohiloliko tayari kuelekeaSyriana kwamba maandalizi yote ya kiufundi na vifaa yamekamilika. Amesema Profesa Åke Sellström ambaye anaongoza jopohilola uchunguzi aliloliunda mwezi uliopita, anaelekeaCyprus.