Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DPRK iache vitendo vya kichochezi: Ban

DPRK iache vitendo vya kichochezi: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema ana taarifa ya uwezekano wa kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu waKorea, DPRK inajiandaa kufanya jaribio la nyuklia. Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini The Hague, Uholanzi, Bwana Ban amesema hata hivyo hana taarifa mahsusi juu ya sualahilokwa wakati huu lakinikamaambavyo amerejelea asubuhi ya leo ya kwamba amekuwa akiisihi DPRK ijizuie kufanya vitendo vinavyoweza kuchochea hali mbaya. 

(SAUTI YA BAN)

“Nimeionya pia serikali ya DPRK ya kwamba vitisho vyovyote kuhusu silaha za nyuklia hakuna maana yoyote ni wakati wa pande zote husika kusaidia kumaliza mvutano na kuanzisha mashauriano ili masuala yote ambayo hayajapatiwa ufumbuzi yaweze kusuluhishwa kwa amani.”

Bwana Ban amesema ni matumaini yake kuwa nchi hiyo itazingatia maazimio ya baraza la usalama nahiloni ombi la dharura kutoka kwa jumuiya ya kimataifa na yeye binafsi.