Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Margaret Thatcher hatunaye tena:

Margaret Thatcher hatunaye tena:

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Baronnes Thatcher amefariki dunia

 (SAUTI YA MARGARET THATCHER)

Rais wa Baraza , mara kwa mara tumezungumza  dhdi ya ugaidi, lakini bado kuna nchi miongoni mwetu ambazo zinahifadhi na kuwapatia mafunzo magaidi, na nyingine ambazo ziko tayari kuunga mkono ugaidi badala ya mazungumzo ya amani. Huu ni usaliti mkubwa dhidi ya Katiba ya Umoja wa Mataifa.”

Ni sauti yake Bi Margaret Thatcher akizungumza katika kikao cha 40 cha baraza kuu la Umoja wa mataifa la mwaka 1985. Amekufa Jumatatu asubuhi kutokana na ugonjwa wa kiharusi. Alikuwa ni mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu Uingereza na aliyehudumu kwa muda mrefu, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 87. akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo hicho Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema

(SAUTI YA BAN)

"Alikuwa kiongozi mwanzilishi katika kutafuta amani na ulinzi hususan wakati wa vita baridi. Pia alikuwa mfano kama waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa Uingereza ambaye siyo tu alidhihirisha uwezo wa uongozi bali pia alitoa matumaini makubwa kwa wanawake wengi juu ya usaw na  usawa wa kijinsia bungeni. Tuna deni kubwa kwake na natumai uongozi wake utakuwa chachu kwa watu duniani kote kwa ajili ya amani, ulinzi na haki za binadamu.”

Thatcher alizaliwa mwaka 1925 na alikuwa waziri mkuu kuanzia 1979 na kuondoka madarakani mwaka 1990 baada ya miaka 11.Na Uingereza kwenye mbali ya kughubikwa na simanzi ya msiba huo anazungumziwa vipi? Solomon Mugera ni mkuu wa masuala ya habari katika shirika la BBC

(SAUTI YA SOLOMON MUGERA)